![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjxJxZ5lNhUufjzdZzGgB5p62a1GVOlPfCOw8OIEDMotf5J1_OtEKvjVM0O8oN5ZTWdxSDEhEKCU5RE9of2cGZFsfX8SOCOwfumLlpQ0u8Gdy3YhJOVkoqzwhAfrcFMDJ8lt30IP3i5Bck/s1600/3.jpg)
Badhi ya wajumbe wa Bunge maalum la Katiba walio katika Umoja wa UKAWA jioni ya leo wameamua kutoka nje wakati wajumbe wakiendelea na majadiliano ya taarifa za kamati ya bunge hilo kuhusu sura ya kwanza na ya sita.
Hatua
hiyo imefikiwa na wajumbe hao baada ya kuunga mkono mchango wa Profesa
Lipumba ambaye amesikitishwa na jinsi mjadala wa bunge hilo
unavyogubikwa na ubaguzi.
Profesa
Lipumba amesema wanahitaji katiba itakayo hakikisha kila mwananchi
anapata haki yake bila kujali rangi jinsia na makabila msingi alioucha
baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere.
Aidha
Profesa Lipumba alieza kuwa amesikitishwa na Kauli iliyotolewa na
Waziri William Lukuvi wakati wa sherehe ya kumsimika mchungaji Joseph
Bundala kuwa Askofu akimwakilisha Waziri Mkuu.
Msikilize hapa:
No comments: